Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Simiyurrh)

Historia ya Hospitali

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ilizinduliwa rasmi na Rais  wa Jamuhuli ya Muugano wa Tanzania ,Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli mnamo 08 Septemba 2018. Hospitali hii inamilikiwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto. Iko eneo la Nyaumata, Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. Hospitali hii inahudumia na kupokea Rufaa kutoka wilaya tano katika Mkoa wa Simiyu na kuhudumia idadi ya watu zaidi ya milioni 1.8 katika Mkoa. Wagonjwa wanaletwa kutoka ngazi ya chini ambayo ni pamoja na hospitali za wilaya na vituo vya karibu vya afya. Majengo mengine bado yapo chini ya ujenzi na kukamilika kwake kutaleta uboreshaji wa huduma zaidi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu. Wengine ni Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luaga Mpina, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthon Mtaka, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Andrew Chenge, Mbunge wa Chemba Juma Nkamia.