HOSPITALI YA SIMIYU YAPOKEA MASHINE YA KUTENGENEZA MAZAO YA DAMU
Posted on: September 28th, 2022
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU umepokea mashine ya kutengeneza mazao ya damu ambayo itasaidia upatikanaji wa mazao mbalimbali ya damu kulingana na uhitaji wa mgonjwa
Afisa Ubora (Qualit officer) kutoka damu salama kanda ya ziwa ,Bw. Emmanuel Ndaki wakati akitoa mafunzo kwa watumishi ikiwemo wataalamu wa maabara alisema mashine hii itasaidia sana katika kuwahudumia wagonjwa wenye uhitaji wa damu ambao mchangiaji wa damu mmoja anaweza kusaidia wagonjwa Zaidi ya mmoja kwani damu kutoka kwa mchangiaji mmoja itaweza kutoa mazao ya damu Zaidi ya moja.
“Kwasasa mtaweza kutengeneza mazao ya damu hapa Hospitalini bila kutegemea mazao ya damu kutoka damu salama kada ya ziwa “ alisema Afisa ubora
Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Frederick Mlekwa alisema ni faraja na furaha kupokea mashine hii ambayo itasaidia sana upatikanaji wa mazao ya damu katika Hospitali yetu ili kuokoa maisha kwa wagonjwa wetu.
“Tumefurahi tumepata mafunzo ya nadharia kwa watumishi ,mafunzo ya vitendo kwa wataalamu wa maabara ya kutengeneza mazao ya damu ,hii italeta chachu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu” Alisema Kaimu Mganga Mfawidhi