HOSPITALI YA SIMIYU YATEMBELEA BMH KUJIFUNZA
Posted on: September 25th, 2022
Viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU tarehe 23/09/2022 wameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamini Mkapa (BMH) jijini Dodoma kwaajili ya kujifunza namna ya kutoa huduma bora kwa mteja.
Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi (DNS )wa BMH, Sr. Sheilla Mnenegwa, amesema ni faraja na furaha kuona Hospitali nyingine zinakuja BMH kujifunza namna ya Kuhudumia mteja.
"Tumefurahi kuwapokea watoa huduma wenzetu waliokuja BMH kujifunza namna bora ya kuhudumia mteja" alisema DNS