KITI CHA HUDUMA ZA MENO 'DENTAL CHAIR' KIMEFUNGWA HOSPITALI YA RUFAA SIMIYU
Posted on: November 19th, 2019Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu imepokea kiti kwa ajili ya kutolea huduma za kinywa na meno (dental Chair) na imekamilisha ufungwaji wake jana tarehe 19/11/2019.
kiti hicho kilitolewa kwa msada wa wizara ya afya na kuletwa Hospitalini Hapo na MSD kitasaidia katika kupunguza adha ya wateja waliokuwa wakipelekwa katika Hospitali jirani ya Somanda ili kupata huduma hiyo.
Hospitali ya Rufaa inazidi kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu
kwa sasa Hospiali inao wataalamu wawili wa huduma za kinywa na meno na ambapo mmoja kaenda masomoni kwa ajili ya kusomea masomo ya shahada ya kinywa na meno
mkuu wa kitengo hicho ndugu Daudi Bukuku alisema kuwa Kupiga mswaki kwa ufanisi walau mara mbili kwa siku huondoa mabaki ya chakula kinywani ambayo husababisha kuoza kwa meno. mabaki haya hutengeneza ute laini unaoganda kwenye sehemu mbalimbali za jino/meno huku ukiwa na mamilioni ya vimelea vya magonjwa (bakteria), hivyo watu wote wazingatie namna bora ya utunzanji wa kinywa na meno yao