MAFUNZO YA WATUMISHI WAPYA (INDUCTION COURSE) TOKA MKAPA FOUNDATION
Posted on: May 15th, 2020Serikali imeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo Watumishi wake ili kutimiza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuongeza nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu, Dr Matoke Muyenjwa alipokuwa akifungua mafunzo kwa waajiriwa wapya 17 toka Shirika la Mkapa Foundation
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu, Dr Matoke Muyenjwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya watumishi wapya toka Mkapa Foundation katika ukumbi wa mikutano wa Hopsitali
Kiongozi huyo amesema utoaji wa mafunzo hayo utasaidia kutoa maarifa mapya, ujuzi na ueledi katika kuwahudumia wateja na kuongeza tija katika kutekeleza majukumu mbalimbali Pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi.
Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Afisa Utumishi Mkuu ndugu Protace T Magayane , yalilenga kuwapitisha watumishi hao katika mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia muundo, Maana na umuhimu wa OPRAS, Mawasiliano thabiti ya Mtumishi wa Umma kwenye Taasisi, Mavazi ya staha kwa Mtumishi wa Umma, Elimu ya magonjwa ya dharura, Maadii ya wa Mtumishi wa Umma, Uandaaji wa mihtasari mbalimbali, Utendaji kazi kwa pamoja (Team Work), Dhana YA 5S KAIZEN, Dhana ya kutembea pamoja, Matumizi bora ya Mifumo na vifaa vya TEHAMA serikalini, Umuhimu wa utunzaji wa takwimu, Namna ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya mripuko mf Corona na Uandaaji wa ripoti mbalimbali.
Mwezeshaji, Afisa Utumishi Mkuu, Ndugu Protace T. Mgayane akiwapitisha watumishi kwenye mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya watumishi wapya
katibu wa Afya Bi Getrude Mhimbi akiwapitisha washiriki wa mafunzo katika mada ya Utekelezaji wa majukumu kwa kuzingatia muundo.
watumiishi wapya wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo yao
Mafunzo hayo yalifungwa na Daktari Bingwa macho Dkt Juma Katwale na kuwaeleza washiriki wote kuzingatia mambo yote waliyoyapata katika mafunzo hayo
picha: Dkt Juma Katwale akifunga mafunzo ya watumishi wapya
picha ya pamoja ya watumishi wapya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo hayo