Makabidhiano ya Hospitali ya Rufaa Simiyu
Posted on: November 17th, 2019
Makabidhiano hayo yalihusisha utiaji saini wa nyaraka za makabidhiano ambapo Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Simiyu Dr Matoke Muyenjwa alimuwakilisha Katibu Mkuu- Afya.
Jambo hili kisheria limefanyika mbele ya viongozi mbalimbali wa serikali, Timu ya uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, mwakiliishi toka wizara ya fedha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, timu ya uendeshaji wa shughuli za afya Mkoa na viongozi toka Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dkt. Matoke Muyenjwa alisema kuwa Makabidhiano hayo sio mwisho wa ushirikiano kwani wataendelea kufanya kazi kwa Pamoja kama ilivyo Kauli mbiu ya Wizara ya Afya "Tutetembee pamoja' na aliendelea kwa kutoa shukurani kwa viongozi wa Mkoa hususani Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Mh Sagini kwa kuongeza eneo la ekari 18 katika eneo la Hospitali na kulifanya eneo hilo kuwa na jumla ya ekari 80 na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji kukubali kupima eneo hilo kwa haraka
"Nawapongeza wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyohudumia wagonjwa, wakati mwingine huwa napita usiku kwa kuwa ni karibu na ninapoishi, lakini attension ya vijana wale katika kuhudumia wagonjwa iko vizuri sana na nawasihi waendelee na moyo huo kwa masirahi mapana ya nchi yetu " alisema Mhe. Jumanne Sagini
"Kwa vituo vyetu vyote tulivyojenga tumeviwezesha na kuwafundisha watumishi, na hivyo Wafanyakazi wazembe wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine.Hospitali ya Somanda malalamiko ni mengi lazima kufanyike mabadiliko, watumishi wabadilike watakaokaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, Hatutaki watumishi wa Afya waingiliwe katika majukumu yao, ila watoe huduma kama walivyofundishwa na wazingatie viapo vyao .Watumishi wawe Wabunifu ikiwezekana waweke 'FAST TRACK' kwani Wapo Watanzania ambao wapo tayari kulipia huduma bora. Watumishi wayapende Maeneo wanayofanyia kazi, wayatunze na kuyafanyia ukarabati utakaodumisha na kuboresha mazingira.Vituo vya Somanda na ikindilo vinatakiwa vifanye mabadiliko katika utendaji kazi wao" Alisema Mh Jumanne Sagini
Mjumbe wa bodi ya Hospitali ya Rufaa alimalizia kwa kutoa Shukurani kwa Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala katika kutekeleza jukumu la makabidhiano na kuahaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa huduma za afya Mkoani Simiyu.