shirika la afya duniani WHO limethibitisha kupatikana kwa chanjo ya Ebola itakayotumika katika nchi zilizohatarini zaidi mwa ugonjwa huo
Posted on: November 14th, 2019Shirika la Afya Duniani (WHO) limedhibitisha kwa mara ya kwanza kupatikana kwa chanjo ya Ebola . hatua hii muhimu itasaidia kuharakisha utoaji wa leseni na upatikanaji wa chanjo hiyo katika nchi zilizo hatarini Zaidi mwa ugonjwa huo. Huu ndio mchakato wa haraka kabisa uliowahi kufanywa na WHO kwa Kuhakikisha kuwa chanjo hiyo inakidhi viwango vya WHO kwa ubora, usalama na ufanisi. Mawakala wa Umoja wa Mataifa wanaweza kununua chanjo hiyo kwa ajili ya kutumiwa na nchi zilizo hatarini zaidi kulingana na pendekezo hili la WHO.
"Hii ni hatua ya kihistoria katika kuhakikisha watu walio na uhitaji mkubwa wanapata chanjo hiyo ili kuokoa maisha," alisema Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus,
Pia Mkurugenzi Mkuu wa WHO alisema "Miaka mitano iliyopita, hatukuwa na chanjo wala matibabu ya ugonjwa wa Ebola. Pamoja na kuwepo kwa chanjo na matibabu ya majaribio, Ebola sasa inazuilika na inaweza kutibiwa. "
Chanjo ya Ebola yenye jina la Ervebo, inayotengenezwa na Merck (kampuni hii inayojulikana kama MSD kwa nchi zilizo nje ya Amerika na Canada). Imeonyeshwa kuwa na ufanisi katika kuwalinda watu dhidi ya virusi vya Ebola katika nchi ya Zaire