UPANDAJI WA MITI YA KIVULI NA MATUNDA HOSPITALI YA MKOA WA SIMIYU WALETA MADHARI YA KUVUTIA
Posted on: November 20th, 2019Wafanya kazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa wa Simiyu wameshiriki katika zoezi la upandaji wa miti ya kivuli na matunda katika eneo la mazingira ya Hospitali. Zoezi hililimefanyika leo tarehe 25/11/2019 likiongozwa na Afisa Afya Mazingira wa Hospitali Bi Glory Stanley Mndasha
Bi Glory aliendelea kwa kusema kuwa miti huchangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa mvua ambayo ina umuhimu mkubwa katika Maisha yetu ya kila siku kwa kutupatia Maji safi na kukuza mazao mashambani. Ukosefu wa mvua kwa muda mrefu hupelekea Ukame na Baa la Njaa katika jamii . Miti hutunza vyanzo vya maji. huleta hewa safi ya oksijeni na husaidia kupunguza Kabonidaioksaidi(hewa ukaa) kutoka katika Mazingizra tunayoishi. Pia miti hutoa Madawa mbalimbali yanayotumika Kutibu Magonjwa mbalimbali,na husaidia sana katika kukinga upepo,Na hivyo huepusha athari zaidi ya Upepo mkali. Pamoja na hayo miti Huifanya ardhi ishikamane na hivyo kuzuia mmomonyoko wa udongo. MIti ya matunda hutupatia chakula (matunda) ambayo hutumiwa na binadamu pamoja na wanyama wengine
"Tumepanda miti 60 ya matunda ambayo ni mchanganyiko wa miembe, miparachichi na michungwa na miti 50 ya kivuli pamoja na maua mbalimbali kuzunguka eneo la Hospitali, Ni vyema kutumia kipindi hiki cha mvua katika kupanda miti ili iweze kustawi vizuri kwa kupata maji ya kutosha, hatua hii muhimu itasaidia katika kutunza mazingira yetu" Alisema Bi Glory Mndasha
wafanya kazi wa SUMA -JKT wakisaidia zoezi la upandaji miti
Afisa Afya Mazingira wa Hospitali Bi Glory Stanley Mndasha akitekeleza zoezi la upandaji miti