Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Simiyurrh)

Wananchi wa mkoa wa Simiyu wafurahia huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya uzazi

Posted on: November 8th, 2019

Na Hierceinter H Silyimbo

Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wamefurahia huduma ya vipimo na uchunguzi wa magonjwa ya uzazi na vizazi iliyokuwa ikifanyika toka tarehe 21-25 Oktoba 2019 katika viwanja vya sabasaba marufu kama viwanja vya CCM wilayani Bariadi-Simiyu. Katika uchunguzi huo jumla ya wateja 671 walihudumiwa .

Wateja 592 walipimwa maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi na kati yao, wateja 25 walikutwa na maambukizi hayo na kuanzishiwa dawa.

Katika uchunguzi wa magonjwa ya siyo ya kuambukiza , wateja 647 walihudumiwa na 24 kati yao walikutwa na shinikizo la damu. Pia wateja 265 walipimwa hali ya lishe ambapo wateja zaidi 25 walikutwa na uzito wa juu na wateja 6 walikutwa na uzito wa chini.

Pia wateja 118 walichunguzwa kansa ya matiti na kati yao watu 4 walikutwa na uvimbe kwenye matiti.

Wateja 335 walichunguzwa saratani ya shingo ya kizazi, wateja 29 walikutwa na viashiria ambapo walipata matibabu.