Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Simiyurrh)

Dharura

Posted on: December 21st, 2024

Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD)

Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD) ni Idara inayopokea rufaa na kesi zote za dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu .. Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD) inatoa huduma kwa wagonjwa walio na mashaka ya kuhatarisha maisha. Malengo ya idara hii ni kuhakikisha wagonjwa wenye mashaka ya kuhatarisha maisha wanahudumiwa na kufanyiwa ufuatiliaji wa karibu kabla ya kuhamishiwa katika wodi za wagonjwa wa ndani kulingana na hali zao.

Kazi za msingi za idara

1. Sehemu ya Triage

Kupokea rufaa na kesi zote za Dharura.

Kukusanya takwimu na tathimini ya upesi kwa hali ya mgonjwa ili kuipa kipaumbele na Kuanzisha matibabu yanayostahili.

Kuwahamishia wagonjwa eneo linalofaa la EMD na  Matibabu.

Kwa wagonjwa ambao hawaitaji huduma ya dharura, wanapelekwa  Idara ya magonjwa ya nje.

2. Ushauri na eneo la Matibabu.

Kutibu wagonjwa kwa vipaumbele kulingana na hali zao pamoja na ufuatiliaji wa afya zao ndani ya masaa 4

Wagonjwa Watapata Ushauri wa Daktari, huduma za kiuguzi kulingana na kipaumbele.

Wagonjwa wanalazwa wodini au kuruhusiwa kulingana na hali yao.