Kitengo cha tiba na matunzo (CTC)
|
Huduma zinazotolewa ni upimaji wa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI,
Kuanzisha kwa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI, ushauri na nasaha na matibabu ya magonjwa nyemelezi.
|
Famasi
|
Kitengo hiki kinahakikisha upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vifaa vya uchunguzi na matibabu.
|
Kitengo cha mionzi
|
kitengo hiki kinahakikisha utoaji wa huduma za X-ray na Ultrasound
|
Kitengo cha Maabara
|
Kutoa huduma za maabara kwa utambuzi wa magonjwa, upimaji na utoaji wa ushauri wa kitaalam ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa mgonjwa
|
Kitengo cha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa
|
Kushughulika na usajili wa mgonjwa, kutunza kumbukumbu za mgonjwa, uainishaji wa takwimu za kitabibu
|
Kitengo cha fedha
|
Hushughulika na usimamizi wa fedha na ripoti zinazohusiana na fedha
|
Kitengo cha manunuzi
|
Hushughulika na manunuzi yote yanayofanyika Hospitalini.
|
Kitengo cha TEHAMA
|
Kinahusika na mifumo yote inayotumika Hospitalini
Mifumo hiyo ni kama GOT HOMIS,GePG pamoja na intaneti
|
Kitengo cha ufuaji
|
kitengo hiki kinahusika na ufuaji wa shuka zinazotumiwa na wagonjwa.
|
Kitengo cha Afya na Mazingira
|
Kitengo hiki kina husika na Utunzaji wa mazingira ya Hospitali, matengenezo ya mfumo wa maji taka pamoja na usimamizi wa taka zinazozalishwa hospitalini.
|
Ustawi wa jamii
|
Kutoa ushauri na msaada wa kijamii, kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa unyanyasaji wa kijinsia
Kutoa msmaha wa matibabu kwa wateja wasiojiweza
|