Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(Simiyurrh)

BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU YAKUTANA

Posted on: January 23rd, 2020


Bodi ya Ushauri (HAB) ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu jana wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Hospitali  katika kikao cha kawaida cha kujadili masuala mbalimbali ya Hospitali kwa kipindi cha robo ya kwanza na pili ya mwaka wa fedha 2019/2020

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali  Bw  Gigi obeid (Aliyesimama)  akiongoza kikao cha bodi hiyo kilichofanyika hapo jana tarehe 22/01/2020.

Mwenyekiti  alifungua kikao kwa kuanza kwa kuwakaribisha wajumbe wote na kisha kumruhusu Katibu wa Bodi ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Dkt  Matoke Muyenjwa  kupitia muhitasari wa bodi wa kikao kilichopita na kujadili maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho.

Aidha taarifa ya kikao cha Bodi ya Afya ya Hospitali na katibu  Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bw Jumanne Sagini  kilichoketi mwishoni mwa mwezi Agosti 2019 ilisomwa na kujadiliwa pia. Bodi ilipitia mapendekezo na maazio ya kikao hicho  ambayo yalikuwa ni  ununuzi wa jenereta kubwa (standby jenerator) ambapo Katibu Tawala alielekeza Hospitali ifanye ufatiliaji wake  na hadi sasa Jenereta kubwa ya uwezo wa KBA 250 imefungwa, ununuzi wa mashine za maabara na hadi sasa mashine za maabara toka bohari kuu ya dawa MSD zimepokelewa,  upatikanaji wa mtandao wa mawasiliano  wa uhakika kupitia njia ya fiber toka TTCL, Ujenzi wa wodi za kulaza wagonjwa, na upatikanaji wa usafiri wa uhakika toka mjini bariadi hadi eneo la Hospitali kwa wateja na watumishi pia.

Baada ya hayo Mwenyekiti alimkaribisha tena katibu ili aweze kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Hospitali  kwa kipindi cha miezi sita toka mwezi Julai hadi Desemba  kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020

Naye Dkt Muyenjwa(Katibu wa bodi)  aliwasilisha taarifa yake na kusema kuwa katika mwaka wa fedha 2019/2020 Hospitali ilipanga kutekeleza shughuli 93 zilizokuwa  kwenye mpango kazi (Comprehesive Hospital Operational Plan) na hadi kipindi  cha nusu mwaka wa fedha 2019/2020, jumla ya  Shughuli 69 sawa na asilimia 74.2% zimetekelezwa, kati ya hizo shughuli kuu zilikuwa ni ununuzi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vifaa vingine vya Hospitali.

“ Uendeshaji wa shughuli mbalimbali za hospitali ikiwa ni pamoja na kulipa stahiki na motisha kwa watumishi, maji, umeme,Vibarua, gharama za matengenezo ya vifaa tiba, miundombinu na magari ambapo hadi kufikia mwezi Desemba 2019 hakuna mtumishi anayedai fedha za sare, malipo ya muda wa ziada wa kazi na wala stahiki nyingine” alisema Dkt Muyenjwa

Aidha Hospitali ya Rufaa kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2019/2020  iliendesha Kliniki tembezi za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni pamoja na  uchunguzi wa magonjwa ya kina mama na uzazi ambapo jumla ya watu 2203 walihudumiwa. Pia Hospitali ilifanya usimamizi elekezi katika kituo cha afya Mwandoya na Hospitali ya Wilaya Meatu  pamoja na kutoa huduma kwa wateja ambapo   jumla ya wateja 189 walihudumiwa na kati ya hao wateja 5 walifanyiwa upasuaji

Dkt Muyejwa aliendelea kwa kueleza kuwa  Jumla ya wagonjwa wa nje 3887 na wa ndani 924 walihudumiwa kwa kipindi cha miezi 6 , na  kati ya hao kulikuwa na vifo 26. Na kwa sasa Hospitali kwa kiasi kikubwa inatoa huduma za wagonjwa wa nje

Hospitali inaendelea na Kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya majengo ya Maabara, Radiolojia, Upasuaji Mkubwa, Kichomea taka na jengo la Mama na Mtoto, uandaaji wa Mpango kazi wa Hospitali na Taarifa mbalimbali za  kila mwezi na robo mwaka na kuziwasilisha katika mamlaka husika,

Jengo la upasuaji mkubwa na Radiolojia

picha: jenereta kwa ajili ya matumizi ya Hospitali

picha: muonekano wa ndani kwenye chumba cha maabara kuu ya Hospitali

picha: ujenzi wa jengo la mama na mtoto

Hospitali imezidi kupata mafanikio mbalimbali ambapo huduma zimezidi kupanuliwa kwa kuongeza vyumba vya kulaza wagonjwa wa kiume, akinamama,  watoto, dharula, kitengo cha macho,Meno na chumba maalumu (Private). Kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 79 kwa robo ya kwanza (Julai – Septemba) na kufikia asilimia 82.5 kwa robo ya pili (Oktoba – Desemba). Na Upatikanaji wa dawa za msingi (tracer medicine) ni Zaidi ya asilimia 97.  Pia hospitali inatumia mifumo ya kuhifadhia  taarifa za wateja kwa  kutumia GoTHoMIS na Mfumo wa kukusanya fedha za serikali (GePG),

Hospitali imefanikiwa  Kununua Generetor,Dental chair,mfumo wa kujisajiri watumishi (Biometric Machine),Mashine za vipimo vya Maabara na Sampuli,Mashine za Jengo la Mionzi(Ultra-sound na X-ray Machine) Vifaa vya Jengo la upasuaji kwa thamani ya Zaidi ya Milioni 313 

licha ya mafanikio mbalimbali hospitali inakiri kuwepo kwa changamoto ya Ukosefu wa  transforma kubwa yenye uwezo wa kusambaza umeme katika majengo yote ya Hospitali.,Upungufu wa vitanda kwa ajili ya kulaza wagonjwa.,Upungufu wa maji kwa ajili ya matumizi ya  Hospitali.,Ubovu wa Miundo mbinu ya barabara kutoka barabara kuu (Bariadi-Ramadi) kuja Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Ukosefu wa uzio wa kuzunguka Hospitali, aidha eneo la hospitali halijakamilika kufidiwa na kupimwa

Picha: Mganga mfawidhi Dkt Matoke Muyenjwa (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Shughuli mbalimbali za Hospitali katika kipindi cha miezi sita

Aidha wajumbe wa bodi walipata wasaa wa kupita katika sahemu mbalimbali za kutolea huduma na kutembeea majengo mapya ya upasuaji mkubwa, radiolojia na maabara.

Picha:wajumbe wa bodi wakiangalia maendeleo ya uwekaji wa benchi za kisasa katika chumba cha maabara kuu

Picha: wajumbe wa bodi wakiwa katika wodi chumba cha wodi maarum (VIP word)

Wajumbe pia walishiriki zoezi la kupanda miti ikiwa ni kumbukumbu na ishara ya kuendeleza utunzaji wa mazingira

picha: wajumbe wa bodi wakipanda miti kuzunguka mazingira ya Hospitali