HOSPITALI YA SIMIYU YATARAJIA KUPOKEA VIFAA KWA AJILI YA MACHO
Posted on: November 16th, 2019wajumbe wa shirika la Briten Holden Institute wameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu na kuongea na timu ya uendeshaji wa shughuli za hospitali (HMT) katika Ofisi ya Mganga Mfawidhi na kuhaidi kuisaidia Hospitali hiyo kwa kuleta vifaa vya macho vitakavyotumika katika kliniki za macho za kila siku pamoja na upasuaji wa magonjwa ya macho. Vifaa hivyo vimeahidiwa kuletwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha ujao.
Kiongozi wa timu hiyo Dr Moes Nassa alisema kuwa shirika lao litazidi kuendelea kushirikiana na wataalamu wa tiba za macho waliopo hospitalini hapo ili kuendelea kutoa huduma za kibingwa za macho.
pia waliahidi kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu hao waliopo Hospitalini ili kuweza kutoa huduma bora za matibabu ya magonjwa ya macho.
Timu hiyo iliendelea na zoezi a upimaji wa magonjwa ya macho katika kituo cha afya cha Muungano kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo wateja zaidi ya 160 walihudumiwa na kupewa miwani na dawa bure