HOSPITALI YA SIMIYU YATOA MAFUNZO KWA KAMPUNI YA USAFI SUMA JKT
Posted on: September 26th, 2022
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa SIMIYU Leo tarehe 27.09.2022 wametoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa kwa watumishi wa Kampuni ya usafi ya SUMA JKT.
Mratibu wa maboresho Dkt. Patricia Mbwasi na Kaimu Afisa Afya Bw. Saimon Sospeter wameelezea namna ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko kama EBOLA , Kaimu Afisa Afya aliwaeleza watumishi hao kuwa wao ni sehemu ya watumishi wa Hospitali wako kwenye hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa , hivyo ni vizuri wakafuata taratibu za kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuchanja chanjo ya homa ya ini na UVIKO 19.
"Tumewapa elimu Leo , kila mmoja anatakiwa kujua magonjwa ya mlipuko kama tulivyowafundisha ikiwemo EBOLA na unapoona dalili au mtu ana dalili za EBOLA unatakiwa kutoa taarifa haraka ili hatua za kiafya ziweze kuchukuliwa " alisema Afisa Afya