KAMPENI YA KUZUIA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA YAZINDULIWA MKOANI SIMIYU
Posted on: November 18th, 2019Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (katikati) amezindua kampeni za kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza Mkoani Simiyu. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 22/11/2019 katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Bw. Sagini amewaasa wananchi wote kupunguza uzito kwa kufuata ulaji unaofaa, kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kuzingatia kanuni bora za maisha ili kuweza kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
PiaMganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange alisisitiza kwa kutoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kufanya mazoezi na kuepuka ulaji wa chakula usiofaa( kula vyakula vyenye mafuta, chumvi na sukari nyingi), ili kuepuka na kudhibiti magojwa yasiyoambukiza ambapo amebainisha kuwa kutofanya mazoezi na ulaji usiofaa kunachangia kwa zaidi ya asilimia 60 magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo kubwa la damu, magonjwa ya akili na saratani za aina mbalimbali.
Uzinduzi huo umehusisha shughuli mbali mbali za upimaji wa presha, kisukari, uzito,ukimwi na malaria pamoja na kufanya michezo mbali mbali kama vile uvutaji kama, kukimbiza kuku kwa wanaume na wanawake, kukimbia mbio fupi za mita 100 ambapo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu Dr Matoke Muyenjwa aliibuka kidedea katika mbio hizo kwa kundi la wanaume.
Katika shindano la mpira wa miguu timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ilichuana na timu ya Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu na kutoka 1-0 na timu ya Hospitali ikatoka kidedea katika mashindano hayo
Maadhimisho haya yalihitimishwa kwa kufanya mazoezi mepesi ya viungo ambapo watu wote walishiriki katika jambo hilo
Hata hivyo watu wote wamehamasishwa kushiriki katika mazoezi yatakayokuwa yakifanyika siku ya jumamosi kila juma la pili la kila mwezi kuanzia saa 12 asubuhi
mazoezi ya pamoja katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza
mchezo wa mpira uliopigwa kati ya timu ya Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu na timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa simiyu ambapo timu ya Hospitali ya Rufaa iliibuka kidedea kwa gori moja bila