Timu ya mashabiki wa Yanga vs mashabiki wa Simba zatoka 2-2
Posted on: November 9th, 2019Timu ya Mashabiki wa Yanga dhidi ya Mashabiki wa Simba toka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu zimetoka sare ya 2-2 kwa mechi iliyochezwa hapo jana tarehe 9/10/2019katika uwanja wa mpira wa Nyaumata Simiyu
"Hatukuwa na mazoezi ya kutosha kuweza kuwashinda wapinzani wetu" alisema Ezekiel Shilikale Ambaye ni Kocha wa timu ya Mashabiki wa Yanga.
"Mechi hizi za mpira ni mazoezi tosha katika kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza" alisema mratibu wa huduma za tiba Hospitalini , Dr Ntugwa Nyorobi.