Maabara
Posted on: December 7th, 2024Parasitolojia
Sehemu hii inawajibika kwa utambuzi wa viumbe vingi vya vimelea katika mkojo, choo na damu. Kwa utambuzi wa Malaria mbinu zote za haraka na za kawaida hutumiwa
Hematolojia
Sehemu ya hematolojia inawajibika kwa kuainisha sampuli za wagonjwa wanaotakiwa na waganga kama picha kamili ya damu (FBP) kwa wagonjwa ili kujua sababu ya ugonjwa , kiwango cha chembechembe za damu, upimaji wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi, homa ya ini na Kaswende. Sehemu hii ndiyo inayowajibika kwa kutoa damu salama kwa wagonjwa wote wanaohitaji damu ndani ya hospitali